Click here for the English version / Bofya hapa kwa toleo la Kiingereza

Mti wa CBET

Mti huu wa CBET ni mfanano kwa mfumo wote wa CBET. Ni picha (ya kuona), bango na hukutaarifu kuhusu vipengele muhimu vya CBET. Miundo yote imefunikwa kwa plastiki (lamination), (muundo wa) A4 na A3, hivyo, inaweza kuwekwa kwenye ukuta katika skuli/shule au kutumika katika vipindi vya mafunzo kwa ajili ya walimu na uongozi.

Mafunzo ya Utangulizi kuhusu CBET

Walimu wa Vituo vya Mafunzo ya Amali na Taasisi za Ufundi walipata Mafunzo ya Utangulizi juu ya ‘nini CBET na namna ya kuwezesha Mafunzo ya Kuzingatia Umahiri? Mafunzo haya ya siku nne kwa makundi 7 ya walimu kutoka Unguja na Pemba. Zingatio lilikuwa ni kuhusu dhana ya CBET (Nini na kwanini?), ujuzi wa kutumia mbinu chochezi (vipi?) na maendeleo ya kazi za vitendo na shughuli za mwongozo wa kazi (ubunifu).

Siku ya 1 Dhana ya CBET

Katika siku hii ya kwanza, washiriki wanajifunza kuhusu CBET na kupata uelewa wa mabadiliko ya dhana kuelekea CBET, ilifafanuliwa katika mada ya 5. Wanabainisha athari za mabadiliko hayo kwa kutathmini taasisi yao wenyewe, ambao hufanya changamoto kubwa zionekane. Wanaweka malengo na shughuli zao kwa kipindi kinachofuata.

Siku ya 2 Mbinu chochezi

Washiriki wanatafakari kuhusu mbinu wanazotumia katika madarasa yao. Wanapenda mbinu zipi na kwa nini? Wanajifunza kuhusu mbinu za kuwezesha kwa njia ya CBET na kupata uelewa wa mabadiliko ambayo yanapaswa kufanywa. Wanatayarisha sehemu ya somo kwa njia ya vichocheo na kufanya mazoezi katika kikundi. Kwa pamoja washiriki wote wanatoa mrejesho ‘Nini kilikuwa kizuri?’ na ‘Ni nini kinaweza kuboreshwa?

Siku ya 3 Kazi za vitendo

Washiriki wanapata uelewa wa haja ya kufanya mabadiliko kutoka katika nadharia kwenda kwenye kazi za vitendo zaidi, zinazohusiana na mahitaji ya soko la ajira. Wanapata uelewa katika vigezo vya muundo, hufanya mazoezi ya muundo wa mgawo wa kazi za vitendo katika vikundi vidogo na kutafakari juu yao katika kikao.

Siku ya 4 Maendeleo ya Kazi

Katika siku hii ya mwisho washiriki wanafahamiana na programu ya ‘Maendeleo ya Kazi’. Katika vikundi vidogo wanachagua zoezi moja kutoka katika mada na wanazifanyia mazoezi kwenye kikundi. Mwishoni kuna tathmini ya mafunzo na kupanga mipango ya utekelezaji na kutoa dondoo namna ya kufanya hivyo.