Click here for English / Bofya hapa kwa toleo la Kiingereza

Shuguli

Katika programu ya Ulimwengu Wangu wa Kazi, iliyofanywa Zanzibar, zaidi ya washiriki na wadau 100 walihusishwa katika shughuli moja au zaidi katika sehemu hii ya mradi wa VNA.

Katika kipindi cha kwanza shughuli zilikuwa:

  • Mkutano wa uongozi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi (Amali) na Vituo vya Mafunzo ya Ufundi (Amali);
  • Siku nne za Mafunzo ya utangulizi kuhusu CBET: makundi manne ya walimu katika ujenzi, viwanda na utalii kwa Unguja na Pemba;
  • Mikutano ili kujadili mapendekezo kwa maendeleo ya sanduku la zana Ulimwengu Wangu wa Kazi;
  • Mafunzo ya siku tatu katika ushoni kwa makundi ya wanafunzi kutoka Manakwerekwe na Mkotoni, pamoja na kazi za vitendo ‘Nguo nzuri, iliyobuniwa na kutengenezwa kwa ushirikiano’. Mafunzo na mashindano haya yalitolewa na wabunifu, Aida A. Suleiman, kutoka Ushirika wa Wanawake wa Sasik kwa ushirikiano na VSO.

Kati ya vipindi viwili kazi katika meza ilifanyika nchini Uholanzi kuendeleza sanduku la zana Ulimwengu Wangu wa Kazi, kwa msaada wa wafasiri kadhaa wa kujitolea.

Katika kipindi cha pili shughuli visiwani Zanzibar zilikuwa:

  • Mkutano wa kuzindua sanduku la zana na kujadili utekelezaji;
  • Mafunzo ya Wakufunzi (T-o-T) kuhusu CBET kwa wale walimu ambao wameshafuata Mafunzo ya Utangulizi kuhusu CBET: siku nne;
  • Mafunzo ya Utangulizi kuhusu CBET kwa kundi kubwa la walimu katika Mafunzo ya Ufundi (Amali), Taasisi za ufundi na washauri kutoka Kituo cha Taifa cha Rasilimali ya Walimu: siku nne;
  • Mafunzo ya siku nane juu ya programu ya Maendeleo ya Kazi kwa walimu, washauri na wakufunzi ambao wanaunga mkono vijana katika kazi zao, kwa njia moja au nyengine.

Wadau na washiriki

Wadau na washiriki ambao walibadilishana mawazo yao, kutoa msaada wao au kushiriki katika shughuli moja au zaidi zilitoka kwa:

  • Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, WKUWVWW
  • Idara ya Ajira (Kazi), Vijana na Ajira
  • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Amali), WEMA
  • Tume ya Mipango, Zanzibar
  • Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi (Amali), MMA
  • Kituo cha Mafunzo ya Ufundi (Amali) Vitongoji, Pemba
  • Kituo cha Mafunzo ya Ufundi (Amali) Mwanakwerekwe
  • Kituo cha Mafunzo ya Ufundi (Amali) Mkokotoni
  • Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, KIST
  • Kituo cha Usindikaji
  • Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, NACTE
  • Taasisi ya Maendeleo ya Utalii Zanzibar, ZiToD
  • Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere – Zanzibar
  • Taasisi ya (kiteknolojia) ya Teknolojia ya Biashara – Zanzibar
  • Kitengo (Skuli) cha Afya cha Zanzibar, Zanzibar
  • Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, SUZA
  • Kituo cha Taifa cha Rasilimali ya Walimu – Zanzibar (NTRSC)
  • Baraza la Vijana Zanzibar
  • Kituo cha Mafunzo KAWA,
  • Practical Permaculture Institute Zanzibar, PPIZ
  • Milele Foundation
  • Ushirika wa wanawake wa Sasik – Zanzibar
  • Kanga Kabisa
  • Kampuni ya Ujenzi ya Rans
  • Randstad Netherlands
  • Hoteli ya MaruMaru
  • Vigor
  • VSO Tanzania