Click here for the English version / Bofya hapa kwa toleo la Kiingereza

Programu ya Maendeleo ya Kazi: namna ya kuwaongoza vijana kwenye mafunzo ya ufundi na ajira au ajira binafsi?

Programu ya Maendeleo ya Kazi huwawezesha walimu wa skuli za sekondari, wakufunzi wa taasisi za mafunzo ya ufundi, kampuni, taasisi zisizo za kirerikali, wizara ya Kazi, Ajira, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Amali) kuchagua mazoezi ambayo yanafaa kwa mahitaji na kiwango cha makundi yao ya vijana.

Programu hailengi kwa vijana kufanyia kazi kwa kujitegemea, bila mwongozo wowote. Bila shaka, washiriki hupata kazi au kazi fulani ya kufanya mmoja mmoja, lakini kwa jumla, hii ni programu ambayo inahitaji mwingiliano, ushirikiano katika makundi na mrejesho. Haiwezi kufuatwa bila mwongozo. Hakikisha unatoa daftari ambalo washiriki wanaweza kuandika na kuhifadhi matokeo na maendeleo yao. Kwenye gamba la daftari, unaweza kuweka mwelekeo wa kazi au washiriki wanaweza kubuni ukurasa wao wa mbele. Walimu na wakufunzi wanahitaji kujiandaa vizuri, na inapendekezwa kwamba mwanzo watafakari maendeleo yao wenyewe ya kazi. Kwa njia hii, walimu na wakufunzi pia ni mfano wa kuigwa katika kuendesha kazi yao wenyewe kiundani.

Mahiri sita za kazi na dira ya kazi

Programu ‘Maendeleo ya Kazi: namna ya kuwaongoza vijana kwenye mafunzo ya ufundi na ajira au ajira binafsi?’ imeundwa karibu na mahiri sita ambazo ni muhimu wakati unapotaka kuendeleza kazi yako:

  1. ‘Gundua kipaji chako’: tafakuri kuhusu uwezo, kupitia umahiri wako mwenyewe kwa heshma ya kazi yako;
  2. ‘Gundua shauku yako’: tafakuri kuhusu hamasa, kupitia matakwa na maadili yako mwenyewe kwa heshima ya kazi yako;
  3. ‘Gundua ulimwengu wako wa kazi’: utafutaji wa ajira, mwelekeo kuhusu maadili na umahiri wako kulinganisha na kinachohitajika katika hali ya kazi za kitaaluma;
  4. ‘Gundua mtandao wako’: mtandao, kufanya na kudumisha mawasiliano ambayo ni muhimu kwa kazi yako;
  5. ‘Gundua biashara yako’: utafutaji wa ajira binafsi, mwelekeo juu ya matarajio na umahiri wako kuanza biashara au kuendeleza kazi kama mjasiriamali;
  6. ‘Mpango kazi wako na kuomba kazi’: udhibiti wa kazi, mipango inayohusiana na kazi na ufafanuzi binafsi wa nafasi kwa mchakato wako wa kujifunza na kazi.

Kila umahiri wa kazi umeshikamanishwa sambamba na swala la kazi na jumla ya mahiri sita zinawakilishwa kama usukani wa uendeshaji wa kazi. Unahitaji kuendesha hatua zako za kazi muda wote kutafuta mwelekeo sahihi. Katika maelezo ya kina ya kila moja ya mahiri sita za kazi, unaweza kupata ufafanuzi zaidi kuhusu umahiri unaouhitaji kufanya kwa vitendo, kuendeleza kazi.

Namna ya kutumia programu kwenye Maendeleo ya Kazi?

Kila umahiri wa kazi unaweza kufunzwa kwa kufanya mazoezi kadhaa. Mazoezi hutofautiana katika maudhui na katika mbinu pia. Hii ni nzuri, kwa kuwa kuna njia zaidi ya moja ya kujifunza umahiri wa kazi.

Mwanzoni mwa kila mada mpya, utakuta maelezo ya jumla ya mazoezi yote ambayo ni ya mada maalum. Katika maelezo hayo ya jumla, kawaida unakuta: jina (kichwa) cha zoezi, lengo na muhtasari wa mbinu chochezi ambazo zinaweza kutumika katika zoezi hili. Kwa njia hii, unaweza kuangalia kwa haraka mazoezi yote na hii itakusaidia kufanya uchaguzi unaokufaa na kundi lako. Uchaguzi mzuri ni ule unaohusiana na maswala ya maendeleo ya kazi ambao wanafunzi, watafutaji wa kazi na wabunifu wa kazi wanao.

Baada ya kuchunguza maelezo ya jumla, unaweza kuvuta mazoezi uliyochangua. Yote kati yao yana muundo sawa. Kwa njia hii, unaweza kuona kwa urahisi namna ya kuandaa na kutoa zoezi kwa njia inayofaa.

Kwa kufanya uteuzi wako mwenyewe, walimu na wakufunzi wanaweza kubuni programu ya mafunzo. Unachagua mazoezi yale ambayo yanafaa kwa mtaala, ratiba ya vipindi vya kozi na kiwango cha wanafunzi/watafutaji wa kazi na wabunifu wa kazi. Uchaguzi unaofanya pia hutegemea na maswali ambayo wanafunzi/watafutaji wa kazi na wabunifu wa kazi wanayo kuhusu kazi yao.

Walimu na wakufunzi wanaweza pia kuchagua yale mazoezi wanayopenda kusomeshea. Baadhi ya mazoezi na mbinu zitakufaa zaidi kuliko nyengine. Vidokezo vinavyotolewa mwishoni mwa maelekezo, ni mapendekezo ili kuwezesha zoezi liwe vizuri iwezekanavyo, lakini jisikie huru kulifanya kwa njia tofauti unazodhani zitakufaa au vizuri zaidi kwa kundi lako.

Bila shaka, unaweza kuongeza mazoezi yako mwenyewe kwenye programu hii. Kwa njia hii, sanduku la zana litakua na kwa kubadilishana mazoezi na wengine, mwongozo wa kazi utatolewa kwa njia nzuri zaidi kwa vijana wa Zanzibar na Tanzania.

Muundo sawa katika mazoezi yote

Mazoezi yote yanaelezwa kwa kina zaidi, kufuata muundo huo huo. Hii itakusaidia kuandaa na kuwezesha mazoezi uliyoyachagua.

Muundo ni:

Lengo: Ni lipi madhumuni ya zoezi? Matokeo gani yatakuwa yanatarajiwa. Kuangalia ufahamu, tabia, ujuzi na vitendo?

Maandalizi: Kama mwalimu/mkufunzi, nini cha kufanya katika maendeleo ya kazi kwa ajili ya kutoa zoezi kwa namna ya kuzingatia mchakato? Jinsi ya kuandaa darasa kuwapa washiriki wako eneo wanalohitaji ili kufanya mazoezi? Baadhi ya mazoezi yanahitaji eneo zaidi au mpangilio tofauti wa viti/meza.

Maelezo: Kama mwalimu/mkufunzi, nini unaweza kuwaambia wanafunzi/watafutaji wa kazi wako na wabunifu wa kazi kama ni utangulizi kwenye zoezi?

Utendaji: Ni nini wanafunzi/watafutaji wa kazi na watoaji wa kazi watalazimika kufanya au kuonesha katika zoezi hilo? Hapa, unaweza kupata mlolongo wa hatua ambazo washiriki huchukua ili kukamilisha zoezi.

Tafakuri: Mwaswali gani unauliza mwishoni mwa zoezi (au baada ya hatua mahsusi wakati wa zoezi)?

Dondoo: Vitu ambavyo unahitaji kuwa na uelewa navyo wakati wa zoezi.

Uchunguzi wa kina: Nini kinaweza kufanywa zaidi kulipa zoezi (kwenda) kina zaidi au kuliunganisha na zoezi jengine?

Karatasi za zoezi: Misaada ya kujifunza, malighafi na vifaa ambavyo vinaweza kutumika na wanafunzi/watafutaji wa kazi na wabunifu wa kazi.

Mazoezi yaliopangwa katika mada sita

Mazoezi ya programu yamepangwa katika mahiri sita za kazi, ambazo zinaitwa ‘mada’ sita.

Mada ya 1 ‘Gundua kipaji chako’

Katika mada ya 1 utakuta mazoezi 20 kuhusu umahiri wa kazi ‘Gundua kipaji chako’: tafakuri kuhusu uwezo.

Gundua kipaji chako inamaanisha: kufikiria kuhusu sifa zako na namna ya kuweza kutumia sifa hizo kuendeleza kazi yako. Wanafunzi/watafutaji wa kazi na wabunifu wa kazi hutafakari juu ya sifa wanazotumia katika maisha yao ya kila siku, skulini na katika kazi (zisizo rasmi). Huwataka wengine (wahitimu, walimu, wanafunzi wenzao, waajiriwa, wajasiriamali na wanafamilia) kuwapa marejesho pale wanapofanya vizuri na pa kuboresha.

Katika maelezo ya jumla Mada ya 1 ‘Gundua kipaji chako’ unaweza kukuta baadhi ya mazoezi ambapo washiriki watapata kujuana kila mmoja na mazoezi ambapo huchunguza maeneo yao walio na nguvu (uweledi). Katika maelezo ya jumla, unapata viunganisho kwa mazoezi tofauti hivyo unaweza kujifunzia kwa kina. Kutoka hapo unaenda kwenye karatasi za zoezi.

Mada ya 2 ‘Gundua shauku yako’

Katika mada ya 2 utakuta mazoezi 14 kuhusu umahiri wa kazi ‘Gundua shauku yako’: tafakuri kuhusu hamasa.

Gundua shauku yako inamaanisha: kufikiria kuhusu matarajio yako na maadili ambayo ni muhimu kwa kazi yako. Wanafunzi/watafutaji wa kazi na wabunifu wa kazi wanakuwa na uelewa ya kile wanachodhani ni muhimu katika maisha yao, elimu na kazi yao. Watagundua kinachowapa hisia za kuridhika, wanachopenda au wasichopenda na kile ambacho (bado) wanahitaji kuendeleza kulingana na matarajio yao.

Katika maelezo ya jumla Mada ya 2 ‘Gundua shauku yako’ unaweza kubofya kwenye mazoezi tofauti kwa maelezo zaidi na kutoka hapo hadi kwenye katarasi za zoezi.

Mada ya 3 ‘Gundua ulimwengu wako wa kazi’

Katika mada ya 3 utakuta mazoezi 24 kuhusu umahiri wa kazi ‘Gundua ulimwengu wako wa kazi’: utafutaji wa ajira.

Gundua ulimwengu wako wa kazi inamaanisha: chunguza mahitaji na maadili ya sasa na baadaye katika taaluma unayotaka. Wanafunzi/watafutaji wa kazi na wabunifu wa kazi huendeleza ujuzi ili kutafuta ajira ambayo inaenda sambamba na maadili yao binafsi. Hujifunza namna ya kutafuta usawa kati ya viwango vilivyopo/maadili ya sehemu ya kazi na vipaji/maadili yao binafsi. Utafutaji wa ajira ni juu ya kupata ladha ya uhalisia ya ulimwengu wa kazi.

Katika maelezo ya jumla Mada ya 3 ‘Gundua ulimwengu wako wa kazi’ unaweza kubofya kwenye mazoezi tofauti kwa maelezo zaidi na kutoka hapo hadi kwenye katarasi za zoezi.

Mada ya 4 ‘Gundua mtandao wako’

Katika mada ya 4 utakuta mazoezi 21 kuhusu umahiri wa kazi ‘Gundua mtandao wako’: mtandao.

Gundua mtandao wako inamaanisha: kutambua mtandao wako, kuujenga na kuudumisha, hivyo unaweza kuendeleza kazi yako kwa njia nzuri iwezekanavyo. Wanafunzi/watafutaji wa kazi na wabunifu wa kazi huendeleza ujuzi kutumia mtandao wao kwa namna ambayo mwanzoni kabisa wanaweza kupata sehemu katika soko la ajira na kwa baadae wanaweza kuudumisha au kuubadilisha. Hujifunza namna ya kuwasiliana kuhusu wakitakacho na wanachohitaji kwa ajili ya kazi yao.

Katika maelezo ya jumla Mada ya 4 ‘Gundua mtandao wako’ unaweza kubofya kwenye mazoezi tofauti kwa maelezo zaidi na kutoka hapo hadi kwenye katarasi za zoezi.

Mada ya 5 ‘Gundua biashara yako’

Katika mada ya 5 utakuta mazoezi 24 kuhusu umahiri wa kazi ‘Gundua biashara yako’: utafutaji wa ajira binafsi.

Gundua biashara yako iamaanisha: chunguza kama ungependa kuanza biashara yako mwenyewe na kuendeleza kazi yako kama mjasiriamaliau mfanya biashara. Wanafunzi/watafutaji wa kazi na wabunifu wa kazi hujifunza maana ya jinsi ya kuishi kiujasiriamali, namna ya kuendeleza maono (malengo ya muda mrefu) juu ya kampuni ya kibiashara wanayotaka kuanzisha na namna ya kujenga ujuzi ili kutengeneza maono hayo imara. Hujifunza kuweka ujasiriamali katika matendo/mwenendo.

Katika maelezo ya jumla Mada ya 5 ‘Gundua biashara yako’ unaweza kubonyeza/kubofya kwenye mazoezi tofauti kwa maelezo zaidi na kutoka hapo hadi kwenye katarasi za zoezi.

Mada ya 6 ‘Mpango kazi wako na kuomba kazi’

Katika mada ya 6 utakuta mazoezi 30 kuhusu umahiri wa kazi ‘Mpango kazi wako na kuomba kazi’: udhibiti wa kazi.

Mpango kazi wako na kuomba kazi inamaanisha: kupanga, kudhibiti na kubadilisha njia yako ya kujifunza na kufanya kazi, kwa nia ya kuboresha maendeleo yako ya kazi. Wanafunzi/watafutaji wa kazi na wabunifu wa kazi huendeleza ujuzi ili kuchukua hatua na majukumu. Hupata ujuzi ili kuchukua, kuweka au kubadilisha nafasi zao katika soko la ajira, hujifunza namna ya kutafuta kazi, namna ya kutengeneza Taarifa Binafsi (Curriculum Vitae), na namna ya kufanya usaili.

Katika maelezo ya jumla Mada ya 6 ‘Mpango kazi wako na kuomba kazi’ unaweza kubofya kwenye mazoezi tofauti kwa maelezo zaidi na kutoka hapo hadi kwenye katarasi za zoezi.