Click here for the English version / Bofya hapa kwa toleo la Kiingereza

Siku ya 1 Utangulizi: kuchunguza kazi yako mwenyewe, mahitaji ya tathmini, vijana na kupanga kazi zako za vitendo

Washiriki wataongeza uelewa kuhusu maendeleo ya kazi yao wenyewe na watafanya tathmini binafsi kuhusu umahiri wao katika kuwaongoza vijana. Wanaweka malengo kuhusu kipi cha kufanikisha na namna ya kuendesha mchakato wao wa kujifunza. Wanafafanua mgawo wa kazi ya vitendo: Tengeneza programu iliyoundwa maalum ‘Maendeleo ya Kazi’ kwa ajili ya vijana unaofanya nao kazi. Na wanaanza na tathmini ya mahitaji ya kikundi cha vijana watakachoongoza.

Siku ya 2 ‘Gundua kipaji chako’

Siku ya 3 ‘Gundua shauku yako’

Siku ya 4 ‘Gundua ulimwengu wako wa kazi’

Siku ya 5 ‘Gundua mtandao wako’

Siku ya 6 ‘Gundua biashara yako’

Siku ya 7 ‘Mpango kazi wako na kuomba kazi’

Siku ya 8 ‘Mawasilisho na Tathmini’

Katika siku hii ya mwisho washiriki wanawasilisha programu yao iliyoundwa kwa meneja, maafisa wakuu na wafanyakazi wenzao wa taasisi zao. Wanaonesha kile ambacho wamefanikiwa na namna maendeleo ya kazi yanavyoweza kuwa sehemu ya mafunzo, kozi na mwongozo ambao taasisi hutoa. Hatimaye kuna tathmini ya mafunzo na kushirikishana kuhusu mahitaji ya utekelezaji na maendeleo zaidi. Na ni aina ya sherehe pamoja na vyeti na duru ya pongezi kwa jirani.